BENEFITS OF BEING A TAPIFA MEMBER

Posted by:administrator in Announcement

BENEFITS OF BEING A TAPIFA MEMBER
Pig Farming in Tanzania is facing a number of challenges which include:
(a) Poor feeding practices among farmers due to high feed prices and insufficient knowledge and skills on appropriate feeds for the various categories of pigs
(b) High costs of Pig Farming inputs, eg Animal scales, Farrowing Crates, etc.
(c) Lack of exotic breeding stock
(d) Lack of modern slaughter facilities
(e) Un-organized market for pork meat and related products
(f) Un-availability of Pig vaccines and reliable medication
(g) Limited availability of qualified veterinarians
In view of the above constraints, a Tanzania Association of Pig Farmers (TAPIFA) has been established with a Mission to serve the interests of Tanzania’s Pig Farmers who are TAPIFA members by promoting and encouraging modern pig farming, research and information dissemination among Pig Farmers and by establishing links with government and all stakeholders in the supply chain in Tanzania as well as globally.

The Vision of TAPIFA is to be a voice and facilitator representing and supporting Pig Farmers in their quest for profitability and sustainability.
Therefore, the benefits of being a TAPIFA member include the following:
1. To possess the right to receive valuable information and assistance on:
    (a) The best and modern pig production techniques, including the best quality of breeds, artificial insemination, their availability and assistance on how to get them in an affordable price;
    (b) Pig feed and formulation;
    (c) Recommended vaccinations and medication and how to get them in an affordable and easy manner;
    (d) Reliable and profitable markets;
    (e) Technical training to be provided to TAPIFA members from time to time;
    (f) Various opportunities in the Pig industry and how to grab them and benefit as an individual farmer; etc
2. TAPIFA will work closely with government bodies and other financial institutions for possible financial assistance to Pig Farmers who are TAPIFA members
    FAIDA ZA KUWA MWANACHAMA WA TAPIFA KWA KISWAHILI
    Kwa muda mrefu wafugaji wa nguruwe wamekuwa na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo kwa uchache:
        (i) Ukosefu wa sera ya serikali ya makusudi na thabiti kuendeleza ufugaji wa nguruwe
        (ii) Ukosefu wa mbegu bora za nguruwe zenye tija
        (iii) Ukosefu wa mafunzo ya ufugaji wa kisasa wenye tija
        (iv) Ukosefu wa soko rasmi la nyama ya nguruwe

        (v) Ukosefu wa dawa, chanjo na pembejeo mbalimbali za nguruwe

Baada ya kukumbana na hizo changamoto wafugaji wachache walioungana na kuunda kundi la whatasap ili kuwakutanisha wafugaji mbalimbali nchini kwa lengo la kuanzisha chama kitakachounganisha wafugaji na kuhakikisha ufugaji wa nguruwe unakuwa na tija. Baadae tarehe 17/09/2016 chama hicho kinachoitwa Tanzania Association of Pig Farmers (TAPIFA) kikaundwa katika mkutano uliofanyika katika hotel ya Nashera mjini morogoro,ukihudhuriwa na wafugaji wapatao 48. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo mwanachama waTAPIFA atafaidika nayo.

1. TAPIFA ni sauti ya wakulima (wafugaji) wa nguruwe katika nyanja zote na inafanya/itafanya kazi na wanachama pamoja na serikali kuhakikisha kuna sera za makusudi na thabiti kuendeleza ufugaji wa nguruwe
2. TAPIFA itahakikisha uwepo wa mbegu bora ya nguruwe nchini
3. TAPIFA itahakikisha wafugaji wanapata mafunzo ya ufugaji nguruwe wa Kisasa. Kutakuwa na mashamba darasa ambapo pia mbegu bora inapatikana
4. TAPIFA itahakikisha soko rasmi la nyama ya nguruwe kwa wanachama wake. Hii ni pamoja na kuanzisha machinjio za kikanda zenye kiwango kinachokubalika na walaji na pia bei nzuri inayotabirika.
5. TAPIFA itafanya kazi kwa karibu na serikali kuhakikisha dawa, chanjo na pembejeo mbalimbali za nguruwe zinapatikana kwa urahisi
6. TAPIFA inafanya na itafanya kazi kwa karibu na taasisi za fedha na wadau mbalimbali kuona jinsi ya kumsaidia mwanachama/wanachama wenye changamoto ya mitaji kupata suluhisho. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

TAPIFA katika umri wake mdogo imeweza kufanikisha yafuatayo
(a) Kupata kampuni inayozalisha mbegu bora za Nguruwe nchini Zambia. Wangwa Farm ni franchise ya Pig Improvement Company (PIC), kampuni ya kimataifa inayozalisha mbegu bora nguruwe aina ya Camborough(kwa majike) na PIC boars(madume). Hadi sasa wanachama wa 25 wameweza kuagiza majike 75 na madume 4 na kuanza kuvuna faida yake
(b) Kupata kampuni nchini Africa Kusini inayoitwa Alliance genetics inayozalisha mbegu bora ya nguruwe aina ya Duroc. Tayari wanachama wameweza kuagiza madume aina ya duroc 5 na majike 3
(c) Kufanya mkutano wa kuanzisha chama ambapo ambapo viongozi walichaguliwa na pia kulikuwa na mafunzo yafuatayo

  • Hali ya nyama nchini ambapo takribani tani2000 za nyama ya nguruwe huagizwa kutoka nje ya nchi. TAPIFA inajizatiti kukidhi soko la ndani na la nje baadae
  • Aina ya mbegu bora duniani na namna ya kisasa ya kuzalisha nguruwe ili kupata nyama bora kwa mlaji

(d) TAPIFA tayari ina akaunti benki kwa ajili ya kukusanya michango ya wanachama.
Jina la Akaunti: Tanzania Association of Pig Farmers
Jina la Benki: NMB
Tawi: Wami-Morogoro
Akaunti namba: 22110037506
(e) TAPIFA ina offisi maeneo ya nanenane –Morogoro na ukarabati unaendelea.

(f) TAPIFA ndio chama pekee cha wafugaji nguruwe kinachotambulika na serikali na taratibu za usajili rasmi zinaendelea.

(g) Kupitia Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, TAPIFA imeweza kuishawishi serikali kuona umuhimu wa sekta ya nguruwe iliyokuwa imesahaulika kwa muda mrefu. Kwa ushawishi huu TAPIFA inatarajia kuingia kwenye mradi mkubwa wa ASDP-Agriculture Sector Development Program na ama miradi mingine mikubwa itayobadili sura ya ufugaji wa nguruwe Tanzania.
(h) TAPIFA ina website rasmi www.tapifa.or.tz

Ukitaka kujiunga na TAPIFA kwa hiari yako fuata taratibu zifuatazo:
1. Tafuta mfugaji ambae ni mwanachama wa TAPIFA na jaza fomu ya kujiunga. Hii fomu ipo pia kwenye website ya TAPIFA
2. Lipia benk Tshs.50,000 amabyo ni ada ya maombi ya uanachama. Hii ada hairudishwi hata kama maombi yako hayatakubaliwa
3. Utajibiwa kama maombi yako yamekubaliwa au la. Ukikubaliwa utahitaji kulipia ada ya kiingilio Tshs.200,000 ili kuwa mwanachama rasmi. Usipokubaliwa waweza pia kuomba kujiunga muda mwingine. Ni vema ukatambua kuwa kila mwaka kutakuwa na ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni Ths.100,000. Ada hizi zaweza kubadilika kadiri uongozi utakavyoona inafaa kila mara.

4. Ukiwa mwanachama utaunganishwa na huduma zote za TAPIFA za wanachama ikiwa ni pamoja kwa sasa na whatasap group la wanachama liitwalo ‘’TAPIFA members” na kuwa na haki zote za mwanachama.